Abstract:
Madhumuni makuu ya ushawishi katika kampeni za uchaguzi ni kukubalika.
Mara nyingi lugha inayotumika katika siasa ina lengo la kusifia au
kulaumu. Lugha hiyo huwa yenye ubunifu, ya kujenga au kubomoa kwani
hutumika kama silaha ya kujilinda. Kwa misingi hiyo, makala hii
inachunguza matumizi ya mbinu za kiisimu katika kampeni za uchaguzi
yanayowezesha kuvuta hisia na kuteka masikio ya hadhira. Aidha, makala
hii inabainisha na kujadili matumizi ya mbinu za kisarufi katika mikutano
ya kampeni za uchaguzi wa Tanzania mwaka 2015. Uchunguzi umeongozwa
na Nadharia ya Balagha na data zimekusanywa kupitia njia ya maktaba.
Makala imebaini kuwa katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015,
wanasiasa walitumia mbinu za uteuzi wa msamiati/istilahi maalumu,
matumizi ya viwakilishi nafsi, ukanushi wa sentensi. Makala inatoa
mchango mkubwa katika kuonesha nguvu ya lugha na ushawishi ya
wazungumzaji wa kisiasa katika kufanikisha malengo yao ya kisiasa
ambayo ni kushinda uchaguzi.