Mwalimu Nyerere Memorial Academy

Institutional Repository

Utohozi wa nomino za kiswahili na athari yake katika ngeli za Kihaya

Show simple item record

dc.contributor.author Adolph, Editha
dc.date.accessioned 2023-06-19T12:46:09Z
dc.date.available 2023-06-19T12:46:09Z
dc.date.issued 2014-10
dc.identifier.citation Adolph, E. (2014). Utohozi wa nomino za kiswahili na athari yake katika ngeli za Kihaya. University of Dar es Salaam, M.A Thesis, Unpublished en_US
dc.identifier.uri http://41.59.91.195:9090/handle/123456789/153
dc.description M.A. Thesis en_US
dc.description.abstract Utafiti huu umechunguza utohozi wa nomino za Kiswahili katika Kihaya na athari yake katika ngeli za Kihaya. Utafiti umefanyika katika kata za Izigo, Mayondwe na Muhutwe wilayani Muleba mkoa wa Kagera nchini Tanzania. Kazi hii iliongozwa na Nadharia ya Mofolojia Leksika ya Kiparsky (1982). Aidha, data ya utafiti huu ilikusanywa kwa kutumia mbinu za hojaji, mahojiano, ushuhudiaji pamoja na njia za uwandani na maktabani. Halikadhalika, mkabala usio wa kiidadi ulitumika katika ukusanyaji na uchambuzi wa data ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa lugha ya Kihaya imekopa baadhi ya nomino kutoka katika Kiswahili. Baada ya nomino za Kiswahili kutoholewa katika Kihaya, zimefanyiwa michakato ya kifonolojia na kimofolojia kadiri ya kanuni na taratibu za lugha ya Kihaya ili ziweze kukubalika katika lugha ya Kihaya. Vilevile utafiti huu umebaini kuwa kuna athari ya kingeli inayotokana na utohozi wa nomino za Kiswahili katika lugha ya Kihaya. Mfano, athari ya nomino za asili za Kihaya kubadili ngeli zake. Aidha, katika utafiti huu inapendekezwa kwamba uchunguzi ufanyike kuhusu mabadiliko ya ngeli yaliyotokea kuanzia zama za Mame-Bantu. Pia, mtafiti anapendekeza maeneo mengine yafanyiwe tafiti, mfano, uainishaji wa lahaja za Kihaya, fonolojia, semantiki, sintaksia na mofolojia ya Kihaya. Aidha, kuna haja ya kufanya uchunguzi tena kuhusu utohozi wa nomino za Kiswahili katika Kihaya kwa miaka ijayo kwani ni wazi kuwa mchakato wa ukopaji na utohozi ni endelevu. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.subject Utohozi wa nomino en_US
dc.subject nomino za kiswahili en_US
dc.subject ngeli za kihaya en_US
dc.title Utohozi wa nomino za kiswahili na athari yake katika ngeli za Kihaya en_US
dc.type Thesis en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search MNMA Repository


Browse

My Account

Statistics